top of page

ADAIWA KUMUUA MKEWE NA KUMZIKA KWENYE CHUMBA WALICHOKUWA WANAISHI...

Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia Mohamed Omary Salahange (37) mkazi wa Rudewa Gongoni wilayani Kilosa mkoani humo kwa tuhuma za kumuua Beatrice Talius ambaye ni Mke wake na kumzika kwenye chumba walichokuwa wakiishi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilio ambapo amesema Jeshi hilo lilipokea taarifa za siri kuhusu mauaji hayo mnamo Machi 21,2024.

Amesema kuwa taarifa za Siri walizopokea zilizoeleza kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo alitenda kosa hilo na kuhama kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na mkewe.

Aidha Jeshi la polisi baada ya kukamatwa mtuhumiwa alikiri kufanya mauaji hayo na kuwa peleka maafisa wa Polisi kwenye eneo la tukio ambapo jeshi la polisi kwa kushirikiana na



wataalamu mbalimbali pamoja na kamati ya usalama wilaya ya Kilosa walifanikiwa kuufukua mwili wa mwanamke kwaajili ya uchunguzi zaidi.

Beatrice ameacha watoto watatu ambapo alizaa na mwanaume mwingine Mkoani Arusha na Kilimanjaro kabla ya kuhamia katika Kijji hicho huku mume wake huyo ambaye ni (mtuhumiwa)hakufanikiwa kupata nae mtoto

Wakati huo Watoto wa marehemu wamekutwa na majeraha ya kung'olewa meno ya mbele.

Kwa upande wao Majirani wanasema baada ya marehemu kutoonekana Kwa muda mrefu mtuhumiwa huyo alikua anatangaza kuwa mke wake ametoroka na laki saba hivyo anamtafuta jambo ambalo sio la ukweli.

Jeshi la Polisi linaendelea na hatua zaidi za uchunguzi wa

kimaabara ili kukamilisha upelelezi kwa ajili ya hatua za kisheria

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page