Na Ester Madeghe,
Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, Ehud Olmart amesema adui mkubwa wa utawala wa Israel sio Iran, Hizbullah wala Hamas bali ni Waisraeli wenye itikadi kali akiwemo waziri mkuu wa sasa wa utawala huo, Benjamin Netanyahu.

Olmart amesema katika mahojiano yake na televisheni ya CNN ya Marekani kwamba "Tunasikitika kwamba Netanyahu anategemea watu wenye itikadi kali na kufumbia macho vitendo vyao visivyokubalika".
Mwezi Mei mwaka jana, Olmert alitoa wito kwa Waisraeli kumiminika mitaani ili kupinga kundi la Netanyahu, Ben Gvir na Smotrich, ambalo alisema linapinga na kutofuata sheria, hali inayoiweka Israel pabaya.
Olmert amesisitiza kwamba "Netanyahu anaishi ndani ya upofu na tope ambalo linamtenga na ukweli, huku akijigamba kuwa yeye na wenzake ndani wanaoungana mkono, kutumia fimbo ya kusema wanapigana kwa ajili ya uwepo wa Israel".
Septemba mwaka jana waziri mkuu huyo wa zamani wa Israel alizusha mjadala mkubwa kuhusu mustakbali wa utawala wa Israel pale alipotahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea vita vya ndani baina ya Wayahudi wanaoshikamana na dini ya wapinzani (maadui) zao.
댓글