top of page

AFARIKI BAADA YA KUPIGWA NA SHOTI YA UMEME AKIDAIWA KUTAKA KUIBA NYAYA ZA UMEME




Kutoka mkoani Manyara Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Adamu Assan (30) mkazi wa Mafichoni Kiteto amepoteza maisha kwa kupigwa na shoti ya umeme akidaiwa kuwa alikuwa anaiba nyaya za umeme.

Marehemu amekutwa chini ya nguzo za umeme zilizobeba transfoma leo April 06. 2024 eneo la Mnadani Partimbo huku akiwa anaonekana kuunguzwa sehemu ya tumboni na umeme

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Manyara Lucas Mwakatundu ameeleza kuwa kabla ya kifo hicho kulikuwa na jaribio la kukata nyaya za umeme na kwamba chanzo cha kifo hicho ni kupigwa shoti ya umeme

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page