top of page

AFARIKI GESTI AKIWA NA MPENZI WAKE..

AFARIKI GESTI AKIWA NA MPENZI WAKE..


Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mahamudu Mbwana, miaka 44, Mkazi wa Mbezi Madale, jijini Dar es Salaam, amefariki dunia akiwa na mpenzi wake, kwenye nyumba ya kulala wageni Ya Another Coast, maeneo ya Mikumbi, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, mkoani Lindi.




Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, ACP Andrew Ngassa, amesema, baada ya mpenzi wake huyo kuhojiwa na polisi, alisema tarehe 26/2/2024, majira ya saa kumi alfajiri marehemu alianza kuishiwa nguvu na kuanza kukoroma.

Polisi baada ya kupata taarifa walifika eneo la tukio na kuukuta mwili wa marehemu, na walipopekuwa nguo zake walikuta dawa ya kulevya aina ya bangi kwenye mfuko wake wa suruali.

Marehemu alikuwa anafanyakazi kwenye kampuni ya Lujuni Costruction Limited, inayojishughulisha na ujenzi wa barabara, na tayari mwili marehemu umekabidhiwa kwa mwajiri wake

Jeshi la polisi wanamshikilia mpenzi wake kwa mahojiano zaidi.

Source: ITV Tanzania

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page