Na VENANCE JOHN
Wizara ya Mambo ya Nje ya Taiwan imesema kuwa serikali ya Afrika Kusini imeipa Taiwan mwisho wa mwezi Machi kuhamisha ubalozi wake kutoka mji mkuu Pretoria.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_a5967355f79b4ebfb6001911c177fada~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_a5967355f79b4ebfb6001911c177fada~mv2.jpeg)
Serikali ya Taiwan, kisiwa ambacho China indai ni sehemu yake kimelaumu agizo hilo, kikisema ni shinikizo la China kwa Afrika Kusini kuchukua hatua hiyo. Afrika Kusini ilikata uhusiano rasmi wa kidiplomasia na Taiwan mwaka 1997 na inadumisha tu uhusiano rasmi, na wa karibu sana na China.
Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Taiwan imesema serikali ya Afrika Kusini ilituma barua mwishoni mwa Januari ikitaka ubalozi wa Taiwan uondoke Pretoria kabla ya mwisho wa Machi na hata kubadilishwa jina kama ofisi ya biashara na sio ofisi ya Ubalozi.
Mahitaji hayo "yanaonyesha ukandamizaji wa China dhidi yetu nchini Afrika Kusini unazidi kuwa mbaya", iliongeza, taarifa ya Taiwan ikisema, hata hivyo, mazungumzo kati ya Taiwan na Afrika Kusini yanaendelea.
Wizara ya mambo ya nje ya China ilisema Afrika Kusini ni rafiki na mshirika mzuri wa China, na nchi hiyo inafanya kile inachopaswa kufanya linapokuja suala la kuzingatia kanuni ya China moja ambayo inasema Taiwan ni sehemu ya China.
China ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika Kusini duniani kote na ambayo inatazamia kupanua ushirikiano katika maeneo kama vile nishati mbadala. Taiwan ina uhusiano rasmi wa kidiplomasia na nchi 12 tu, na barani Afrika ina mshirika mmoja tu aliyesalia, Eswatini, ambayo imezungukwa kabisa na Afrika Kusini.
Comments