Na VENANCE JOHN
Ofisi ya rais wa Afrika Kusini imesema katika taarifa yake kuwa Afrika Kusini imewasilisha ushahidi wa kesi yake ya mauaji ya halaiki dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ). Hati hizo hazitawekwa wazi, na zina zaidi ya kurasa 750 za ushahidi unaoungwa mkono na vielelezo na viambatisho vya zaidi ya kurasa 4,000.

Afrika Kusini mwezi Disemba mwaka 2023 iliishutumu Israel kwa kukiuka sheria za kimataifa kuhusu mauaji ya halaiki wakati wa vita vyake huko Gaza na imeiomba mahakama kuamuru Israel kusitisha vita.
Ushahidi huo unalenga kuonesha jinsi serikali ya Israel inavyokiuka Mkataba wa kuzuia Mauaji ya Kimbari kwa kuendeleza uharibifu dhidi ya Wapalestina wanaoishi Gaza, kwa kuwaua kimwili kwa aina mbalimbali za silaha za uharibifu, na kuwanyima fursa ya misaada ya kibinadamu. Israel mara zote imekataa vikali madai ya Afrika Kusini ikishilia msimamo kuwa inatekeleza sheria ya kimataifa ya kujilinda dhidi ya uvamizi wa nchni yake.
Comments