top of page
Radio on air

AHUKUMIWA MIAKA 10 JELA KWA KUFANYA MAPENZI NA MTU MWENYE CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI...

Kutoka mkoani Songwe Kamanda wa Polisi Mkoani humo, SACP Augustino Senga amesema Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imemuhukumu kifungo cha miaka 10 jela



mshtakiwa Yusuph Laiton Simbeye mwenye miaka 28 mkazi wa Mbozi kwa kosa la kufanya mapenzi na mtu asiye na akili timamu.

Kamanda Senga ameyasema hayo alipozungumza na vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa majukumu yao kwa mwezi Mei na kuongeza kuwa hukumu hiyo ni moja ya mafanikio ambayo jeshi la polisi limeyapata.

Aidha Senga amesema jeshi hilo pia limefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani zaidi ya watuhumiwa 684 kwa makosa mbalimbali ikiwemo ukatili wa kijinsia, mauaji na ubakaji.



Source Via: Azam TV

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page