top of page

AJALI YA ARUSHA VIFO VYAFIKIA 25

AJALI YA ARUSHA VIFO VYAFIKIA 25 NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI ATEMBELEA ENEO LA AJALI NA HOSP...


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini leo Februari 25,2024 amewatembelea na kuwajulia hali majeruhi wa ajali iliyotokea Februari 24,2024 katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Arusha, Mount Meru Arusha

Katika ajali hiyo idadi ya watu waliofariki imefikia watu 25 na majeruhi 21.

Ajali hiyo ilihusisha lori na magari matatu ambapo katika waliofariki, wanaume ni 14, wanawake 10 na mtoto mmoja.

Kamishina wa Polisi, Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Awadhi Juma Haji amesema kati ya waliofariki, watu saba ni raia wa kigeni waliokuwa wakijitolea kufundisha katika Shule ya New Vision waliokuwa kwenye basi la shule.

Miili ya waliofariki imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo, pamoja na Hospitali ya Arusha Lutherani Medical Center Selian.

Yorumlar


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page