top of page
Radio on air

AJALI YASABABISHA VIFO VYA WATU 14 MBEYA...

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera amethibitisha kuwa ajali iliyohusisha magari matatu Jijini Mbeya leo saa saba mchana Mlima wa Simike eneo la Mbembela, imesababisha vifo vya Watu 14 huku wengine 18 wakijeruhiwa.




Ajali hiyo imehusisha Lori namba T.979 CVV likiwa na Tela namba T.758 BEU Scania likiendeshwa na Ross Mwaikambo (40) likitokea Shamwengo likiwa limepakia kokoto, Toyota Coaster namba T.167 DLF na Toyota Harries namba T.120 DER.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema Lori hilo liliendelea kugonga guta namba MC 660 BCR na kisha kugonga pikipiki namba MC 889 CKX "chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva wa lori namba T979CVV/T758 BEU kushindwa kulimudu gari kwenye mteremko, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Dereva wa gari hilo ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya akiwa chini ya ulinzi"


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page