top of page

AJALI YAUA SHABIKI MMOJA WA SIMBA SC, YANGA YATOA POLE

Taarifa kutoka klabu ya Simba SC inaeleza kuwa

"Uongozi wa klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali za mashabiki wetu zilizotokea usiku wa kuamkia leo wakiwa njiani kuelekea Dar es Salaam kushuhudia mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Ajali ya kwanza imehusisha mashabiki wa Tawi la Kiwira Rungwe la mkoani Mbeya ambapo



imetokea katika eneo la Vigwaza, Pwani. Taarifa za awali kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza mtu mmoja amepoteza maisha.

Ajali ya pili ni Tawi la Wekundu wa Border kutoka Tunduma iliyotokea Doma, Mkoani Morogoro. Taarifa kutoka eneo la tukio inaeleza kuwa mtu mmoja ameumia na hakuna madhara makubwa.

Tayari viongozi wa Simba wanaelekea eneo la ajali Vigwaza ili kutoa msaada zaidi kwa waathirika. Uongozi unatoa pole kwa wote walioathir- ika na ajali hizo, familia pamoja na Wanasimba wote kwa ujumla."

Aidha klabu ya Yanga SC imetoa salamu za pole ikieleza

"Uongozi wa Young Africans Sports Club unatoa pole kwa Uongozi wa Simba Sports Club kufuatia msiba wa shabiki wa timu hiyo aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwenye ajali ya gari lililobeba mashabiki waliokuwa njiani kuja Dar Es Salaam kutazama mechi za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu mahala pema peponi. Amen.

Pia, tunatoa pole kwa mashabiki wote waliopata majeraha kwenye ajali mbili, maeneo ya Vigwaza Pwani na Doma, Mkoani Morogoro wapone haraka waweze kurejea katika majukumu yao.

Vilevile, Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuwaomba mad- ereva na mashabiki wote wa soka wanaosafiri kutoka mikoani kuja Dar Es Salaam kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa, kuwa watulivu na kuzingatia alama za usalama wa barabarani wakati wote wa safari.

Tuwatakie safari njema wote na Mwenyezi Mungu azibariki safari zenu Amen".

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page