top of page

AJIUA BAADA YA KUPOTEZA MILIONI 2.3 KWENYE KUBETI KAMARI YA KINDEGE AVIATOR KWA HELA ZA BOSS...

Mshtuko na huzuni umetawala kwa wakazi wa Majengo viungani mji wa Kericho huko nchini Kenya, baada ya mwili wa mwanaume mwenye umri wa miaka 24 kupatikana ukining'inia kwenye paa la nyumba ndani ya chumba alichopanga.




Collins Kipkorir anadaiwa kujitoa uhai baada ya kupoteza pesa za Kenya Sh120,000 (ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 2 za Tanzania) kupitia kamari ya kindege(Aviator) Jumatatu asubuhi.

Kabla ya kifo chake, Kipkorir aliajiriwa kwenye duka la Mpesa ndani ya mji wa Kericho. Inaripotiwa kuwa alitumia pesa za biashara kujaribu bahati yake na kupoteza dau lake katika michezo yote.

Kulingana na ripoti za NTV ya Kenya, Akiongea kwa njia ya simu mpwa wa marehemu Aron Kosgey alisema, "Marehemu alimuomba rafiki yake amuangalizie duka kwani yeye alienda kufanya shughuli kadhaa mjini na atarejea muda mfupi baadae."

"Tulijaribu mara kadhaa kuwasiliana naye lakini hakuwa akijibu simu yoyote," alisema Kosgey.

Kulingana na ripoti ya polisi, hakuna noti yoyote ya kujitoa mhanga iliyopatikana katika eneo la tukio. Mwili huo ulitolewa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Siloam ukingoja uchunguzi wa mwili.

Usiache kufuatilia Msasa Online kwa habari zaidi tembelea tovuti yetu Https://www.msasamedia.com

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page