top of page

AKAMATWA AKIWA NA BUIBUI 300, TANDU 110 NA MCHWA 9 VIKIWA VIMEFUNGWA KWENYE MWILI WAKE

Na VENANCE JOHN


Polisi nchini Peru wamemkamata mwanamume ambapo amekamatwa akijaribu kuondoka nchini humo akiwa na buibui aina ya tarantula 320, tandu 110 na mchwa jamii ya Paraponera clavata tisa wa risasi mwilini mwake.


Raia huyo wa Korea Kusini mwenye umri wa miaka 28 alisimamishwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jorge Chávez mjini Lima baada ya maafisa kugundua kuwa eneo la tumbo lake lilionekana kubwa.


Upekuzi ulifichua mamia ya wadudu waliokuwa wamepakiwa ndani ya mifuko ya ziplock iliyofungwa kwenye tumbo lake. Polisi walimshikilia mtu huyo, ambaye alikuwa akisafiri kwenda Korea Kusini kupitia Ufaransa.


Wadudu hao wanadhaniwa walichukuliwa kutoka eneo la Madre de Dios katika Amazon ya Peru na sasa wako chini ya uangalizi wa mamlaka. Walter Silva, mtaalamu wa wanyamapori anasema buibui aina ya tarantula ambao wana manyoya mwilini mwao ni spishi iliyo hatarini kutoweka.


Peru sio taifa pekee la Amerika Kusini linalokabiliwa na matatizo na usafirishaji wa wanyamapori kwani kwani mwezi Desemba 2021, mamlaka nchini Kolombia ilikamata angalau tarantula 232, mende 67, mayai tisa ya buibui, na nge wakiwa na watoto wake saba, wote wakiwa wamefichwa kwenye sanduku kwenye uwanja wa ndege wa El Dorado huko Bogotá. Na mnamo Septemba mwaka huo maofisa wa Colombia walichukua shehena ya karibu mapezi 3,500 ya papa yaliyokuwa yakienda Hong Kong.

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page