Na Ramla Ramadhan
Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba amesema akiba ya fedha za kigeni Nchini Tanzania katika kipindi hiki kifupi imeongezeka kufikia dola za kimarekani milioni 5,345.5 kwa mwaka 2024

Ameyasema hayo wakati akiwasilisha mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka 2024/2025 bungeni mjini Dodoma Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba amesema kuwa ongezeko hilo limeifanya serikali kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi katika kipindi cha miezi minne mfululizo.
Comments