top of page

ALICHOKIONESHA FREDDY HATUNA BUDI KUSIMAMA NAE ATATUFIKISHA KILELE CHA MAFANIKIO - AHMED ALLY




Kutoka kwa Meneja habari na mawasiliano Simba SC Ahmed Ally amefunguka haya kuhusiana na mshambuliaji wao Freddy Michael

Wakati mwingine Matokeo yasiyoridhisha ya timu huwa yanafifisha ubora wa mchezaji mmoja mmoja au matokeo mazuri ya timu hua yanaficha madhaifu ya mchezaji mmoja mmoja

Fredy Michael Fungafunga tangu amewasili Simba Sports amefunga jumla ya Magoli 10 katika mashindano yote aliyoshiriki ni wastani mzuri sana kwa mshambuliaji.

Champions league 1


Ligi kuu ya NBC 4Kombe la Crdb 4 Kombe la Muungano 1


Imani yangu ni kwamba kadri anavyopata muda wa kucheza, kadri anavyoaminiwa ndivyo anathibitisha ubora wake.

Kwetu sisi Wana Simba jukumu letu ni kumuunga mkono Mshambuliaji wetu na tukumbuke ya kwamba hii ndio nafasi ngumu zaidi kwenye mpira duniani kote.

Kwa alichokionesha Fredy hatuna budi kusamama nae ili atufikishe kwenye kilele cha mafanikio.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page