Na mwandishi wetu @godson2nyi
Mwanamuziki wa Bongo Fleva @officialalikiba ambaye pia ni Rais wa Crown Media ameendelea kutambulisha familia ya kituo chake kipya ambapo kwa kuanza alianza na

Mtangazaji mashuhuri wa vipindi vya burudani Dullah na sasa amemtambulisha aliyekuwa Mtangazaji wa #ManaraTv ya Haji Manara @pablo_almas_7 kuwa Mtangazaji mpya wa Crown Media kupitia ukurasa wa Kiba amefunguka haya
"Kipaji, Ubunifu, Uaminifu, Uchapakazi, Utu na Utulivu vyote unavyo nenda kawahudumie Wana Afrika Mashariki na Kati @pablo_almas_7 Bingwa kweli kweli wa Michezo, Tukio la kwanza tukutane MWANA FA CUP leo, Muheza, Tanga. Karibu @crownfmtz @crowntvtz Hapa Ni Nyumbani."
Kijana huyu amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na uchapakazi lakini pia uwezo alionao hususani katika ufahamu wa matumizi ya Lugha mbalimbali za Kimataifa kama Kingereza, Kifaransa na Kiarabu.
댓글