Na VENANCE JOHN
Kiongozi mkuu wa Syria, Ahmed al-Sharaa aliyeongoza vita ya kumwondoa madarakni rais wa Syria ametangazwa kuwa rais wa Syria kwa muda huu wa mpito. Tangazo hilo limetolewa jana na hivyo Al-Sharaa kuimarisha madaraka chini ya miezi miwili baada ya kufanikisha kampeni ya kumwondoa mamlakani Rais wa muda mrefu wa Syria, Bashar Al-Assad.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_37262dd4db5f4469ae1010dbcc943e4e~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_37262dd4db5f4469ae1010dbcc943e4e~mv2.jpeg)
Maamuzi hayo yalitokana na mkutano wa makamanda wa kijeshi walioshiriki katika shambulio ka kumng’oa Bashar al-Assad mashambuliz yaliyoongozwa na kundi la waislamu la Sharaa la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) ambalo ni tawi la zamani la al Qaeda.
Akihutubia mkutano huo, Sharaa amesema kipaumbele cha kwanza nchini Syria ni kujaza pengo katika serikali kwa njia halali na ya kisheria. Pia alisema amani ya kiraia lazima ilindwe kupitia haki ya mpito na kuzuia maonyesho ya kulipiza kisasi, kwamba taasisi za serikali hasa kati ya vikosi vya kijeshi na usalama zijengwe upya, na kwamba miundombinu ya kiuchumi iendelezwe.
Sharaa ameahidi kuanza kipindi cha mpito cha kisiasa ikiwa ni pamoja na kongamano la kitaifa, serikali shirikishi na hatimaye uchaguzi, ambao amesema unaweza kuchukua hadi miaka minne mpaka kuufanyika. Hata hivyo katika tangazo la hapo jana, haikusemwa ni lini chombo kipya cha kutunga sheria kinaweza kuchaguliwa.
Comments