Na VENANCE JOHN
Mwanamume mmoja nchini Singapore amejikuta matatani baada ya kujaribu kupanga njama dhidi ya aliekua mke wake ambaye walikwisha achana hapo awali. Unaambiwa kesi iligeuka chungu baada ya kuweka bangi kwenye gari la ex wake huyo aliekua mke wake.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_bf67cb8d1a9e438b8d86c892a539c5f9~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_bf67cb8d1a9e438b8d86c892a539c5f9~mv2.jpg)
Tan Xianglong mwenye miaka 37 aliweka zaidi ya nusu kilo ya bangi kati ya viti vya nyuma vya gari la mwanamke huyo, akidhani ilitosha kutoa hukumu ya kifo kwa kosa la ulanguzi wa dawa za kulevya kwa mkewe wa zamani.
Singapore ina baadhi ya sheria kali zaidi duniani za kupambana na dawa za kulevya, ambazo serikali inasema ni muhimu kuzuia uhalifu unaohusiana na dawa za kulevya. Tan Xianglong alijua kwamba kwa kuweka bangi kwenye gari, ingepelekea mhusika kukamatwa na kushtakiwa kwa uhalifu mkubwa ikiwa mpango wake ungefaulu.
Na sasa kibao kimemgeukia mwanaume huyo kwani hapo jana amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu na miezi 10 jela kwa kupatikana na bangi baada ya mahakama kusema ilizingatia shtaka la pili la kupandikiza ushahidi kinyume cha sheria.
Tan Xianglong na mkewe walifunga ndoa mwaka 2021 na kutengana mwaka mmoja baadaye na hawakuweza kuwasilisha talaka kwa sababu Singapore inaruhusu talaka kwa wenzi ambao wameoana kwa takriban miaka mitatu na Tan Xianglong aliamini kwamba angeweza kuondolewa sheria hiyo ikiwa mke wake angekuwa na rekodi ya uhalifu.
Comments