top of page

ALIYEUA WATOTO WAKE KWA SUMU NAE AFARIKI

Mama wa watoto wawili Mario Semen (4) na Beonis Semen (2), Daines Mwashambo (30), aliyewaua wanae hao kwa kuwanyweshwa sumu nae amefariki katika Kijiji cha Mashese Mkoani Mbeya.

Kabla ya umauti huo mama huyo alikuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na tukio hilo la mauaji.


Kamanda wa Polisi Mkoani humo Benjamin Kuzaga amethibitisha kuwa marehemu alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya nae amefariki dunia Machi 9 Saa 10:15 jioni.

Kamanda Kuzaga amesema kuwa marehemu akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Mashese - Ilungu aliwanywesha sumu watoto hao, kisha na yeye alikunywa sumu hiyo iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya matibabu.

Mtuhumiwa aliendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo akiwa chini ya ulinzi, lakini Machi 9 akafariki dunia.

Amesema kuwa uchunguzi wa awali ulibaini kuwa tukio la mama huyo kuwaua wanae na kujaribu kujiunga na yeye imetokana na msongo wa mawazo.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa jamii kuwa pindi unapopatwa na tatizo suluhisho lake sio kujichukulia sheria mkononi bali ni kutafuta ushauri au kufuata sheria inavyoelekeza ili kuepuka madhara kwa muhusika na jamii inayokuzunguka.

Komentáře


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page