top of page

ALLY HAPI KATIBU MKUU MPYA WA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA...

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 03 Aprili, 2024 jijini Dar Es Salaam, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na masuala mengine, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kuwachagua wajumbe kama ifuatavyo




Ndugu John Mongella kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, akichukua nafasi ya Ndugu Anamringi Macha ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Ndugu Amos Gabriel Makalla kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, akichukua nafasi ya Ndugu Paul Makonda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Ndugu Ally Salum Hapi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania, akichukua nafasi ya Ndugu Gilbert Kalima ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga,

Ndugu Jokate Urban Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, akichukua nafasi ya Ndugu Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page