top of page
Radio on air

AMEWASIHI WALE WOTE WENYE MAWAZO TOFAUTI NA HAYO WAFUNGE MJADALA HUO

Taarifa iliyochapishwa kupitia ukurasa rasmi wa Ikulu ya Zanzibar imeeleza kuwa

"Hivi karibuni kumetolewa maoni yanayopendekaza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi aongezewe muda wa kubakia madarakani kwa miaka saba badala ya miaka mitano iliyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar.



Maoni hayo yamekwenda mbali zaidi hata kutaka Uchaguzi Mkuu wa mwakani kumchagua Rais wa Zanzibar usifanyike, jambo hili halina tija wala faida kwa nchi yetu na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye kufuata misingi ya demokrasia.

Rais Dk. Mwinyi ni muumini wa kufuata Katiba na Sheria za nchi, tunapenda kusisitiza kwamba maoni haya si ya Mhe. Rais wala sio ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar

Kwa muktadha huu, Rais Dk. Mwinyi ataendelea kuheshimu utaratibu uliowekwa wa Rais kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Aidha, amewasihi wale wote wenye mawazo tofauti na hayo wafunge mjadala huo."

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page