top of page

ANAYESHIKILIA NAFASI YA URAIS KWA MUDA NCHINI KOREA KUSINI NAYE KUFUNGULIWA MASHTAKA

Na VENANCE JOHN


Chama kikuu cha upinzani nchini Korea Kusini kinapanga mara moja kuchukua hatua za kumshtaki kaimu rais Han Duck-soo, ambaye ni kiongozi mkuu wa chama hicho.


Kiongozi wa ngazi ya chama cha Democratic Party (DP) Park Chan-dae alitangaza hayo baada ya Han Duck-soo, kuahirisha kuidhinisha sheria ya kuanzisha uchunguzi wa mawakili maalum kuhusu jaribio la Rais aliyesimamishwa Yoon Suk Yeol lililofeli la kuweka sheria ya kijeshi. "Kaimu rais Han Duck-soo, aliweka wazi katika mkutano wa baraza la mawaziri la leo kwamba hataangazia sheria maalum ya mashtaka," Park alisema.


Waziri Mkuu Han amechukua hatamu kutoka kwa Yoon aliyesimamishwa kazi, ambaye alitimuliwa Desemba 14, 2024 na anakabiliwa na mapitio ya Mahakama ya Kikatiba kuhusu iwapo itamwondoa madarakani au kurejesha mamlaka yake.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page