top of page

AOKOTA MILIONI 14 CHOONI AZIRUDISHA APONGEZWA KWA UAMINIFU WAKE

Kutana na Mwanamke mwenye Asili ya Marekani na Nigeria arudisha Dola 5,700 (Tsh. Milioni 14.5+) Alizoziokota kwenye Choo za kazini kwake. Kitendo chake kimepongezwa sana na mwajiri wake, wenzake kazini, na Wa-Nigeria wenzake walio ughaibuni.


Bibie Ogunremi alimpata mwenye pesa kabla ya kuarifu uongozi wa kampuni yake. Kitendo chake cha uaminifu kilimfanya apongezwe na wenzake kazini, ambao walimshukuru kwa misimamo yake thabiti ya kimaadili.


Alieleza kuwa maadili yake yanatokana na malezi aliyopata kutoka kwa baba yake aliyefariki, ambaye alifundisha umuhimu wa uaminifu. "Alitufundisha tusichukue kile kisichokuwa chetu. Maadili haya yamekuwa dira yangu katika maisha yangu, na natumai kuyafundisha watoto wangu na wajukuu wangu," alisema Ogunremi.

Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page