top of page

APIGA SIMU KUOMBA MSAADA POLISI BAADA YA KUVAMIWA NYUMBANI KWAKE, KISHA KUULIWA NA POLISI

Na VENANCE JOHN


Mwanamume mwenye umri wa miaka 43, Brandon Durham ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi huko Las Vegas nchini Marekani, baada ya kupiga simu polisi kuomba msaada alipokuwa akipambana na mvamizi nyumbani kwake. Polisi wanasema Durham alipiga simu polisi kuripoti juu ya watu wawili waliokuwa wakifyatua risasi nje huku walikuwa wakijaribu kuingia ndani ya nyumba yake.


Baada ya Afisa wa polisi kufika, alimkuta Durham akiwa hana shati akinyang’anyana kisu na mwanamke aliyefunika uso (ninja), ambaye baadaye alitambuliwa kuwa ni Alejandra Boudreaux mwenye umri wa miaka 31. Kisha Alexander Bookman ambaye ni afisa wa polisi anasikika akipaza sauti, "hey, dondosha kisu, dondosha kisu, sekunde chache baadaye akafyatua risasi iliyompata Durham.


Video ya kamera iliovaliwa na polisi huyo inaonyesha alimfyatulia risasi tano zaidi Durham na kusema weka mikono yako juu. Familia ya Brandon Durham, akiwemo bintiye mwenye umri wa miaka 15 ambaye alikuwa amejificha chumbani wakati wa tukio, wameomba afisa huyo afukuzwe kazi.


Wakili wa polisi huyo, Alexander Bookman, aliyempiga risasi Durham, anasema mteja wake hakufanya uhalifu wowote. Binti mwingine wa Durham anasema inaumiza kwamba polisi wa Las Vegas walimchukulia baba yake kama mshukiwa na sio kama mwathirika.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page