top of page
Radio on air

ASIMWE MTOTO MWENYE UALBINO ALIYEUAWA KAGERA AZIKWA

Kutoka mkoani Kagera mtoto mwenye ualbino Asimwe Novart mwenye umri wa miaka miwili na nusu ambaye ameuawa kwa kukatwakatwa viungo vyake katika eneo la Kamachumu lililopo Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera amezikwa leo June 18,2024 nyumbani kwao Kijiji cha



Bulamula Kata ya Kamachumu Wilayani Muleba.

Mazishi hayo yamesimamiwa na Serikali yakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Kwa mujibu wa Polisi Mkoa wa Kagera, Mtoto huyo alichukuliwa nyumbani kwao May 30 mwaka huu 2024 na mwili wake umepatikana jana June 17 na mpaka sasa Watu wanne wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi akiwemo Baba Mzazi wa Mtoto huyo, mwili wa Mtoto huyo umekutwa umefungwa kwenye mfuko na kutelekezwa kwenye kalavati barabara ya Ruhanga-Makongora kata ya Ruhanga, Tarafa ya Kamachumu huku viungo vyake vikiwa vimekatwa.

Akiongea leo June 18,2024 wakati akishiriki Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari Jijini Dar es salaaam, Rais Samia ameeleza jinsi alivyoguswa kifo hicho ambacho ambapo amenukuliwa akisema "Kuna kifo kimetokea na kimenigusa sana cha Mtoto mdogo alikuwa anacheza akatekwa wakamnyofoanyofoa, siku tatu hakijaonekana kimeonekana kimeharibika, tusimame kwa dakika moja tumuombee"

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page