top of page

ASKOFU MKUU WA ZAMANI WA ANGLIKANA AJIUZULU KWA KUMRUDISHA KAZINI KASISI ALIYEWANYANYASA WATOTO

Na VENANCE JOHN


Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Canterbury Bw. George Carey ameacha utumishi wake kama kasisi wa Kanisa la Uingereza (Anglikana) baada ya uchunguzi wa shirika la utangazaji la Uningereza BBC kufichua kuwa alikuwa akimtetea anayedaiwa kuwa mnyanyasaji wa watoto arejee kuwa kasisi.


Kasisi David Tudor alipigwa marufuku na Kanisa kwa miaka mitano katika miaka ya 1980, kwa madai ya shambulio dhidi ya wasichana wadogo, lakini George Carey baadaye alimruhusu kurudi kuhudumu kama kasisi lakini chini ya uangalizi.


David Tudor alifukuzwa kazi kama kasisi mwezi Oktoba mwaka huu baada ya kukiri makosa ya kuwanyanysa wasichana wadogo kingono. Katika barua yake ya kujiuzulu, George Carey amesema imekuwa heshima kuhudumu kama kasisi kwa zaidi ya miaka 60. Kwa sasa George Carey ni mzee mwenye umri wa miaka 89.


Uchunguzi ulifichua kwamba mwaka wa 1993 George Carey, ambaye wakati huo alikuwa Askofu Mkuu wa Canterbury, alikubali David Tudor arejee kutoka kusimamishwa na kuanza kuhudumu na kwamba George Carey alimsaidia David Tudor kupata kazi.


Zaidi ya hayo, nyaraka zilizovuja pia zinaonyesha alikubali kuondoa jina la David Tudor kwenye orodha kuu ya makasisi waliochukuliwa hatua za kinidhamu. George Carey, ambaye alikuwa Askofu Mkuu wa Canterbury kuanzia 1991-2002, aliwaambia wachunguzi kuwa hakumbuki jina la David Tudor.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page