Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani inaeleza kuwa . "Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Iinamtafuta Abdallah Mohammed miaka 40, fundi Friji mkazi wa Mataya Kata ya Kiromo, Wlaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani kwa tuhuma za Mauaji ya mzazi mwenzake Naomi Mwakajengele maarufu kwa jina la Anangisye miaka 28 mwalimu wa Shule ya Msingi Mataya.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_beb445b1794a4cd49b49b347e5481375~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_beb445b1794a4cd49b49b347e5481375~mv2.jpeg)
Tukio hilo lilitokea tarehe 10/02/2025 majira nane usiku ambapo wawili hao wakiwa chumbani kwao zilisikika kelele toka kwa marehemu Naomi Mwakajengola akidai mwenza wake anamuua ndipo baada ya muda Abdalah Mohammed ambaye kwa sasa ni mtuhumiwa alitoka ndani kwenda chumba dada kazi kumtaka kulala na watoto wawili mwenye umri wa miaka 4 na mwengine miaka 2 ambao awali walikuwa wamelala na marehemu mama yao.
Dada wakazi alishtuka asubuhi baada ya jirani alipokuwa akimuita Abdallah Mohammed huku mlango ukiwa wazi pasi na kufahamu baba wa nyumba aliondoka muda gani kwenda kusikojulikana
Uchunguzi wa awali umebaini mwili wa marehemu kuchomwa na kitu chenye ncha kati ubavu wa kulia, ubavu wa kushoto na kwenye chembe ya Moyo. Awali walikuwa na tofauti ambazo zilipelekea kutokuishi pamoja kwa muda mrefu wawill hao, kabla ya Abdallah Mohammed kurudi tena kwa mzazi mwenzie wiki mbili zilizopita na kutokea kwa tukio hilo.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa wito yeyote atakaemuona mtuhumiwa huyo kutoa taarifa mapema kwa Jeshi la Polisi, viongozi wa Serikali au chombo chochote cha dola ili aweze kukamatwa na hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Comentarios