top of page

AUNTY EZEKIEL AMPA ZAWADI YA GARI MWANAE COOKIE IKIWA NI BIRTHDAY YAKE, ATAJA SABABU

Anaandika @auntyezekiel sababu za kumpa mwanae zawadi ya gari

"Kwanza Kabisa Niseme Ahsante MUNGU KWA ZAWADI HII Ya DADA COOKIE!

Siwezi kuandika Vitu vingi lakini kikubwa ni kwamba Cookie Umekuwa faraja kubwa sana kwenye Maisha yangu Umekuwa chachu kubwa sana ya Mm Kuendelea kusaka Maisha kwa Nguvu kuna Muda uwa sioni faida ya Maisha naona poa tuu ila Mkinijia kichwani Watoto wangu Naamka na KUSALI Mwenyezi Mungu aniongeze japo Uhai kidogo Niwasogeze wanangu



mana Najua DUNIA Sio Rafiki kabisaaa Najua nikiondoka hamtoweza Najua Mtakuwa ila Chamoto utakiona haswa ww mana ndio Dada

Kwenye hii siku yako Niseme tuu Nakupenda sana COOKIE WANG tulipotoka ni mbali Mabonde uko Mgongo raha uko Mgongoni Nachokusihi endelea kuwa Mtoto mzuri hvyohvyp dada Japo kuna Muda changamka kidogo dunia haitaki kuwa mpole zaidi utaonekana bwege!

Tatu hili gari jaman Sijampa kwa Maonyesho au kuwa nina Pesa sanaa HAPANA Tena HAPANA HAPANA HAPANA KABISA! Kilichotokea ni hv Cookie now ni CLASS 4 SO wanatakiwa kwenda shule saa 11 na Nusu Alfajiri School Bus inaanza kufata watoto Saa 12 kwahyo hawa ka nne na la Saba lazma wapelekwe na Wazazi wao

Sio kazi ngumu sana ila kutokana na Mazingira kwangu inakuwa Ngumu kuna Muda nakuwa shooting mara nachelewa kurudi

Time nyingine Nasafiri kabisaa kwahyo nyumbani kunakuwa hamna namna zaidi ya watoto kufatwa na Bajaji kitendo cha Wanangu kupanda Bajaji uwa kinaniumiza Mno kwanza

nakaa Porini sana na hizo story za mara mtoto kalawitiwa

mara hv zilikuwa zinanichanganya mno wakitoka ile 11 silali

nawaza tena haswa kipindi cha Mvua muda mwingine anatoa analia si unajua watoto tena basi Dah! Nikasema No way basi tukajichanga tukasema badala ya

kumfanyia bday party acha tumtaftie kigari chake Apate na dereva ili hii Kero iishe! Thank God nilichowaza kimefanikiwa Mwenyewe alifurahi sana mana nilishampromise kuwa tutamnunulia Gari!ila hakujua lini! Happy Bday Dada Mkubwa Happy bday Chaupole wang Happy bday Roho yangu Yesu waletu aliye Hai akutunze Milele Mama Mama Love u so Much my Sweetheart!"

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page