top of page

AUSTRALIA YATUNGA SHERIA KALI KUPAMBANA NA CHUKI DHIDI YA WAYAHUDI

Na VENANCE JOHN


Nchi ya Australia imeanzisha sheria kali za kukabiliana na uhalifu wa chuki, ikianzisha hukumu za makosa ya ugaidi na kuonyesha alama za chuki, kufuatia mfululizo wa mashambulizi ya chuki dhidi ya Wayahudi katika miji ya Sydney na Melbourne.


Sheria mpya zimepitisha leo Alhamisi ambapo adhabu kali kwa uhalifu wa chuki, ikiwa ni pamoja na kifungo cha kuanzia miaka sita jela kwa makosa ya ugaidi, na angalau kifungo cha miezi 12 kwa uhalifu mdogo wa chuki, kama vile kutoa saluti ya itikadi ya Kinazi (Nazism) hadharani.


Sheria hiyo pia inaunda makosa mapya ya kutishia nguvu au unyanyasaji dhidi ya makundi yanayolengwa na watu kulingana na mwelekeo wao wa kijinsia, utambulisho wa kijinsia, ulemavu, dini au kabila.


Mabadiliko hayo yalipendekezwa kwa mara ya kwanza na serikali ya Waziri Mkuu Anthony Albanese mwaka jana huku kukiwa na ongezeko la mashambulizi dhidi ya Wayahudi (Waisreali) na kutaka wahalifu wapewe adhabu kali zaidi.


Wengi kati ya idadi ya Wayahudi 117,000 nchini Australia wana wasiwasi baada ya mfululizo wa mashambulizi ya chuki dhidi yao katika miji yake miwili mikubwa ya Sydney na Melbourne, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya uchomaji moto kwenye kituo cha kulelea watoto na masinagogi, pamoja na kuchora alama ya swastikas kwenye majengo na magari.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page