top of page

AZAM FC HAWAPOI WASHUSHA STRAIKA LA KAZI KUTIKA COLUMBIA

Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa Azam FC wametoa taarifa hii

"Tunayo furaha kutangaza kwamba tumekamilisha uhamisho wa mshambuliaji raia wa Colombia, Jhonier Blanco, kutoka klabu ya Aguilas Doradas ya mji wa Rionegro, inayoshiriki


Ligi Kuu ya Colombia.

Blanco aliyezaliwa Oktoba 18, 2000, amesaini mkataba wa miaka minne baada ya kufaulu vipimo vya afya, kufuatuatia makubaliano baina ya klabu yake na Azam FC.

Alianzia soka lake kwenye akademi ya Club Deportivo Estudiantil kabla ya kujiunga na timu ya ligi kuu ya Aguilas Doradas.

Akatolewa kwa mkopo kwenye klabu ya daraja la kwanza ya Fortaleza. Akiwa na klabu hiyo, akaibuka kuwa mfungaji bora akiisaidia kupanda daraja. Baada ya mkopo akarudi klabuni kwake Aguilas Doradas hadi sasa ambapo Azam FC imemnunua.

Welcome to Azam FC, @jhonierblanco9!"

Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page