top of page

BAADA YA KIKOSI CHA WALINDA AMANI CHA UN KUJIONDOA WAASI WA M23 WAJIIMARISHA.

.Huko mkoani Kivu kaskazini nchini Kongo, baada ya kikosi cha walinda amani wa umoja wa



mataifa kujiondoa kwenye ngome zao kando na mji wa sake, waasi wa M23 wamejiimarisha kwenye ngome hizo.Hadi sasa hofu imeongezeka katika eneo hilo ambapo makundi ya vijana wazalendo wamekuwa wakilengwa kwa makombora na M23 wanaokuwa sasa kilometa 20 na mji wa GOMA. Huku hayo yakiarifiwa wanajeshi watatu kutoka nchini Tanzania wamekufa baada kuangukiwa na kombora nchini Kongo, waliokuwa sehemu ya kikosi cha Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC kinacholisaidia jeshi la serikali kupambana na waasi hao wa M23.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page