Na VENANCE JOHN
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imethibitisha kuwa waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, wamechukua udhibiti wa mji mkuu wa Kivu Kusini wa Bukavu. Waasi hao wamesema wameuteka mji huo wa mashariki wenye wakazi milioni 1.3 na wenye utajiri wa madini, ili kurejesha hali ya utulivu baada ya kutelekezwa na majeshi ya Kongo.

Msemaji wa muungano wa makundi ya waasi unaojulikana kama Congo River Alliance unaolijumuisha kundi la M23, Bw. Lawrence Kanyuka, amesema vikosi vyao vinajitahidi kuwalinda wananchi na mali zao.
Serikali mjini Kinshasa imeahidi kuwa itarejesha utulivu huko Bukavu, lakini hakukuwa na askari wa Kongo eneo hilo, huku wengi wao wakionekana kujiunga na maelfu ya raia waliokuwa wakiuhama mji huo.
Comments