top of page
Radio on air

BABA ADAIWA KUWANAJISI WATOTO WAKE MAPACHA NA KUWAAMBUKIZA MAGONJWA YA ZINAA MOROGORO.....

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Hamad Kapera (20) mkazi wa Kilosa mkoani



Morogoro kwa tuhuma za kuwanajisi watoto wake mapacha wenye umri wa miaka miwili na kuwaambukiza magonjwa ya zinaa.

Imeelezwa kuwa, tukio hilo la kikatili lilitokea Mei 21 wakati mama yao alipokwenda shambani na kuwaacha watoto nyumbani wakiwa na baba yao na ndipo ukatili huo ulipofanyika.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mwanaume huyo anashikiliwa pamoja na mke wake kwa kosa la kukataa kutoa ushahidi.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa mama wa watoto hao ambaye jina lake limehifadhiwa, alifika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka kuomba mume wake asamehewe ili waendelee kuwalea watoto wao.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page