top of page

BABA AMUUA KWA RISASI BINTI YAKE KWA KUPOST VIDEO ZISIZO NA MAADILI TIKTOK

Na VENANCE JOHN


Mwanamume mmoja ambaye hivi majuzi aliirudisha familia yake nchini Pakistan kutoka Marekani jana Jumatano amekiri kumuua kwa kumpiga risasi bintiye kijana baada ya kutoridhishwa na maudhui (video) yake ya TikTok.


Mshukiwa huyo, aliyetambuliwa kwa jina la Anwar ul-Haq, awali alisema kuwa watu wasiojulikana ndiyo walimpiga risasi na kumuua bintiye mzaliwa wa Marekani, mwenye umri wa miaka 15. Afisa wa polisi Babar Baloch amesema baadaye Anwar ul-Haq alikiri uhalifu huo wa kumuua bintiye.


"Uchunguzi wetu kufikia sasa umegundua kuwa familia ilikuwa na haipendi uvaaji wake, mtindo wa maisha, na namna anavyohusiana na kijamii," mpelelezi wa polisi, Zohaib Mohsin, alisema na kuongeza; “Tuna simu yake. Imefungwa.”


Familia hiyo ilikuwa imerejea hivi majuzi kutoka Marekani na ilikuwa inaishi katika jimbo la Balochistan nchini Pakistan na familia hiyo ilikuwa imeishi Marekani kwa takriban miaka 25. Bintiye Haq alianza kuunda maudhui yanayoweza kupingwa kwenye mtandao wa kijamii wa TikTok alipokuwa akiishi Marekani.


Kulingana na Tume huru ya Haki za Kibinadamu ya Pakistani, zaidi ya wanawake 1,000 wanauawa kila mwaka nchini Pakistani mikononi mwa jamii au wanafamilia kwa kile kinachodaiwa kuwa ni uharibifu wa heshima.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page