top of page

BABA YUPO KAZINI MTOTO ANASHANGILIA UBINGWA..

Unaweza kusema hivyo baada ya baba mzazi wa mchezaji wa Real Madrid Dani Carvajal Ramos ambaye ni Afisa wa polisi kuwa mmoja wa maaskari waliokuwa wanasindikiza basi la



Real Madrid lililokuwa limebeba kombe la UEFA Champions League waliloshinda kwenye uwanja wa Wembley, London, England ili kuonyeshwa mbele ya mashabiki wakati wa mapokezi jijini Madrid.

Ikumbukwe kuwa Dani Carvajal alikuwa ndiye mfungaji wa bao la kwanza kwenye ushindi wa 2 bila dhidi ya Borussia Dortmund kisha kutwaa kombe hilo, huku pia akiibuka mchezaji bora wa mchezo(Man Of The Match).

Baadaye baba yake Dani, Mzee Carvajal Ramos aliweza kupiga picha na kombe akiwa na mtoto wake.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page