top of page

BABUTALE AMPA ISARITO MAUA YAKE "UNAJUA MIMI SIKUJUI ILA NI SHABIKI NAMBA MOJA"

Wanasema mtu mpe sifa zake angali yu hai azipokee najukujua kuna fulani alinipa sifa hizi ila sio nyakati amelala hasikii tena ndio uanze kumwaga sifa kede kede ndio maana Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Hamis Taletale maarufu kama @babutale ameamua kuandika



ujumbe huu kwa muigizaji Isalito Mwakalindile @isarito_tmt

Nimeamka na maua ya Isarito Leo nimechuma maua yenye Oksijeni ya pongezi nyingi Juu ya Kijana Mwenye juhudi ziliandikwa kwa mpango wa jasho.

Acha leo nimpe mauwa yake huyu mwamba japokuwa mimi sijawahi kumuona uso kwa uso, ila nimejikuta tu nakuwa Shabiki yake kwa kile anachokifanya kwenye kila kazi yake ya Sinema.

Ndugu yangu @isarito_tmt najua unajua kuwa Mimi sikujui hata chembe, lakini nataka ufahamu kuwa, Mimi ni Shabiki yako namba moja kwa sasa.

Naomba upige kifua chako na ujue kuwa, Wewe ni Mkali haswaa na nakuona mbali sana katika safari ya heshima na mafanikio.

Kikubwa endelea kusimamia kile ambacho Mungu amekupa kwani naamini lazima kitatoa matunda kwako, familia yako na Nchi kwa ujumla.

Endelea kukaza kwakuwa jasho la haki ya kazi yako litakulipa thamani ya heshima itakayoishi vizazi na vizazi. Ameandika Tale.

Isarito anafanya vizuri sana kwenye tamthilia ya Jua Kali na sasa kwenye tamthilia yake mpya ya Bunji iliyojizolea maelfu ya watazamaji.

Tembelea tovuti yetu www.msasamedia.com upate kusikiliza muziki mzuri, makala bila kusahau kuperuzi taarifa zetu.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page