top of page

BAJETI YA WIZARA YA UJENZI NA VIPAUMBELE VYAKE 2024/25

Wizara ya Ujenzi kupitia kwa waziri Innocent Bashungwa imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 1,769,296,152,000 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2024/25

Kati ya fedha hizo Shilingi 81,407,438,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ya Wizara na Taasisi na Shilingi 1,687,888,714,000 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.


Kati ya fedha za Matumizi ya Kawaida, Shilingi 76,588,233,000 ni za Mishahara ya Watumishi na Shilingi 4,819,205,000 ni za Matumizi Mengineyo.

Bajeti ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inajumuisha fedha za ndani Shilingi 1,141,803,989,000 na fedha za nje ni Shilingi 546,084,725,000 Fedha za ndani zinajumuisha Shilingi 599,756,467,800 kutoka Mfuko wa Barabara na Shilingi 542,047,521,200 ni fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali.

Aidha, waziri Bashungwa amebainisha vipaumbele nane vya Wizara ya Ujenzi itakavyotekeleza katika bajeti mwaka 2024/25 ambavyo ni pamoja na kufanya matengenezo ya miundombinu ya barabara na madaraja iliyoharibiwa na mvua, ujenzi wa barabara za kimkakati, na miradi ya udhibiti wa uzito wa magari, ujenzi na ukarabati wa vivuko kupitia TEMESA na miradi ya nyumba na majengo ya Serikali kupitia TBA,

Vipaumbele vingine vilivyobainishwa ni pamoja na kuendelea na matengenezo ya barabara Kuu na za Mikoa, kuendelea kuwajengea uwezo wataalam wa ndani kwa lengo la kuongeza wataalam wabobezi, mapitio ya Sera ya Ujenzi (2003) na Sera ya Taifa ya Usalama Barabarani (2009) pamoja na kanuni na miongozo mbalimbali.

Pia Bashungwa amegusia suala la Wizara TANROADS inatarajia kuanza kutekeleza mradi wa kimkakati wa Ujenzi wa Daraja la Jangwani. Daraja hilo litakuwa na urefu wa mita 390 pamoja na Barabara unganishi zenye urefu wa mita 710 na kina cha mita 15.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page