Na Ester Madeghe,
Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF) limelaani unyanyasaji wa "kudhalilisha" uliomkumba mwamuzi Jose Munuera Montero kutokana na uamuzi wake wa kumtoa nje kiungo wa kati wa Real Madrid Jude Bellingham.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na Montero wakati wa mechi ya Jumamosi ya sare ya 1-1 dhidi ya Osasuna kwa kutumia lugha chafu. Montero amekuwa akipokea unyanyasaji katika mitandao ya kijamii, huku familia yake pia ikilengwa katika unyanyasaji huo.
Waamuzi na wataalamu wa michezo wamekerwa kabisa na mashambulizi na vitisho ambavyo Jose Luis Munuera Montero anapokea kupitia mitandao ya kijamii. Kiungo wa zamani wa Birmingham City Bellingham amesema lugha yake ilitafsiriwa vibaya na mwamuzi Montero.
"Aliamini kwamba nilisema [kitu cha kumtusi]," amesema Bellingham. "Hakukuwa na nia ya kumtusi, hakukuwa na matusi, na kwa sababu hiyo nadhani unaweza kuona kulikuwa na kutokuelewana." Bellingham kwa sasa anakabiliwa na marufuku ya muda mrefu, katika wakati ambapo Real Madrid imeruhusu uongozi wa pointi saba kuteleza kileleni mwa jedwali la La Liga.
Kikosi cha Carlo Ancelotti hakina ushindi katika mechi zao tatu za mwisho za ligi na sasa wako katika kiwango cha pointi na wapinzani wao Barcelona lakini wako nafasi ya pili kwa sababu wana tofauti ndogo ya magoli.
Comments