Na VENANCE JOHN
Benki za Urusi zilivunja rekodi ya faida ya kila mwaka kwa kupata rubles trilioni 4 sawa na dola bilioni 40.7 mwaka uliomalizika wa 2024. Ukuaji huo unaripotiwa licha ya kuwa Urusi iko katika vita na jirani yake Ukraine toka mwaka 2021.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_825dcb07196f45918e4dcf979c7587a7~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_825dcb07196f45918e4dcf979c7587a7~mv2.jpeg)
Benki kuu ya Urusi leo imesema kuwa, wakati sekta ya kifedha ya Urusi ikiendelea kukumbana na misukosuko kutokana na vikwazo vya nchi za magharaibi, lakini kupanda kwa viwango vya juu vya riba na ukuaji thabiti wa mikopo vimesaidia benki za Urusi kupata faida.
Kiwango cha juu cha benki kuu, ambacho sasa ni asilimia 21, kimeongeza kiwango cha riba cha benki, lakini ukuaji wa mikopo unaanza kupungua huku gharama za ukopaji zikizidi kuzuia baadhi ya makampuni kutafuta ufadhili wa miradi ya maendeleo, badala yake wakipendelea kuweka fedha kwa amana. Hata hivyo Benki kuu tayari imeonya kwamba faida za benki zitapungua mwaka wa 2025 huku hatari za mikopo zikiongezeka.
German Gref, Mkurugenzi Mtendaji wa mkopeshaji mkuu wa Sberbank ametaja viwango vya juu vya riba kuwa changamoto kubwa kwa biashara na benki, wakati Andrey Kostin, mkuu wa benki ya VTB amesema udhibiti mkali pia utakula faida za benki. Mapato ya jumla ya riba ya benki za Urusi yalipanda kwa 11% hadi rubles trilioni 6.7 mwaka 2024.
Comentarios