top of page

BIDEN KUIPA UKRAINE MABOMU YA KUFUKIA ARDHINI

NA VENANCE JOHN


Rais wa Marekani Joe Biden amekubali kuipa Ukraine mabomu ya kufukia ardhini. Mabomu hayo hufukiwa chini ya ardhi hasa eneo la mapigano na hulipuka ikiwa maadui watapita juu ya ardhi yalipofukiwa. Afisa huyo ambaye alizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, anasema mabomu ya aina hiyo yatapelekwa hivi karibuni na Washington inatarajia yatatumika katika eneo la Ukraine.


Afisa huyo amesema Ukraine imeahidi kutotumia mabomu hayo katika maeneo yenye raia wa Ukraine. Hatua hiyo inaonekana kama jaribio la kupunguza kasi ya wanajeshi wa Urusi ambao wamekuwa wakisonga mbele kwa kasi mashariki mwa Ukraine katika miezi ya hivi karibuni.


Utoaji wa mabomu ya ardhini ni hatua ya hivi punde zaidi ya utawala wa Marekani unaomaliza muda wake wa kuimarisha juhudi za vita vya Ukraine kabla ya Donald Trump kurejea Ikulu ya White House tarehe 20 Januari.


Urusi imeyatumia mabomu ya ardhini tangu kuanza kwa uvamizi wake kamili wa Ukraine mnamo Februari 2022 lakini pingamizi za kimataifa za utumiaji wa silaha hizo kwa misingi kwamba zinahatarisha raia zilizuia utawala wa Biden kuruhusu matumizi yake.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page