top of page

"BINTI ANASTAHILI HAKI YAKE" WAZIRI GWAJIMA


Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mh. Dorothy Gwajima amesema ,"Ndugu Wananchi, nimepokea 'Tags' nyingi za maoni na maswali kuhusu taarifa iliyotolewa na RPC mkoa wa Dodoma juu ya mwenendo wa shauri la 'Binti wa Yombo' (rejea taarifa za awali).





Ndugu Wananchi, nimepokea hisia zenu, maoni na maswali yenu ambayo mmeelekeza kwangu. Nimewasiliana na Mhe Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye tayari naye amepokea na anafanyia kazi hivyo, tumpe nafasi atatoa taarifa yake.


Ndugu Wananchi, ni dhahiri kuwa, alichofanyiwa 'Binti wa Yombo' ni kitu kibaya kisicho cha utu hivyo, anastahili haki yake kwa mapana yote. Ndugu Wananchi, Nawasihi tujipe muda na kuamini kuwa, haki itatendeka kwa mujibu wa sheria na itaonekana bayana na siyo vinginevyo."

Yorumlar


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page