top of page

BINTI WA JACOB ZUMA RAIS WA ZAMANI WA AFRKA KUSINI ASHITAKIWA KWA KUCHOCHEA VURUGU

Na VENANCE JOHN


Duduzile Zuma-Sambudla, binti wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma, amefikishwa mahakamani akishtakiwa kwa kuchochea ghasia wakati wa vurugu za mwaka 2021 ambapo zaidi ya watu 300 waliuawa.


Waendesha mashtaka wanadai kuwa Zuma-Sambudla alichochea watu wengine kufanya vurugu kupitia machapisho kwenye mitandao ya kijamii Julai 2021, baada ya baba yake kukamatwa kwa kutotii amri ya mahakama baada ya Zuma kutofika mahakamani kutoa ushahidi katika uchunguzi wa rushwa.


Maandamano juu ya kufungwa kwa Zuma ziligeuka kuwa ghasia, na kusababisha uporaji wa maelfu ya maduka, uharibifu mkubwa wa miundombinu ya umma na vifo vya takriban watu 350. Zuma-Sambudla aliambatana na baba yake Jacob Zuma katika mahakama ya Durban na binti huyo atarudi tena mahakamani mwezi Machi.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page