top of page

BONGO INA WANAWAKE WAZURI MNO NI KUOMBA MUNGU UPATE ALIE SAHIHI KWAKO - MANARA



Kutoka kwa Haji Manara amefunguka haya kupitia ukurasa wake wa Instagram

"Nilipoonana Siku ya kwanza tu nilijisemea moyoni huyu ndio Mke wangu sasa, huyu ndio Mwanamke wa maisha yangu,na kadri siku zilivyokuwa zikisogea nikawa nathibitisha hilo kwenye moyo wangu.

Amenibadilisha kabisa, now zaidi ya kazini kwangu ni home tu,na ikibidi kutoka kokote kule pembeni yangu yupo yeye, Marafiki zangu nikiwakumbuka nawaita home tunafurahia maisha.

Haji mie sina Maskani, Sina Club na siendi kwa Mtu,hii pia ndio mara yangu ya kwanza katika uhai wangu, kukubali na kuridhika mambo ya kupekuliana Simu, nadhani Wakware mshauona moto wake DM. Buga now nakula kwa wakati tena nyumbani, sikuwahi kuwaza Toto tundu kama mimi ntakuja kuishi hivi.

U know what? Ananipa furaha na amani na ndio chanzo cha mabadiliko hayo, naenjoy zaidi kukaa nyumbani kwa sasa kuliko kwenda shopping Beverley Hills.

Kiuhalisia kale kanyimbo kanachoimbwa nalishwa na kudekezwa itakuwa niliimbiwa mimi Bugati.

Eeh Mola wetu karimu na Rahmaani tupe raha mimi na habibt wangu, tuishi hivi hivi kwa furaha, tudumishe katika hii ndoa hadi utakapoanua kumchukua mmoja wetu, na tujaalie masikilizano InshaAllah A

Nb: Bongo ina Wanawake wazuri mno ni kuomba Mungu upate aliosahihi kwako, muhimu kuwapa mapenzi, matunzo kisha kuwajali, hawaimbiwi mdundiko hawa majumbani, hupewa mahaba." Ameandika Manara.

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page