top of page

BONGO MOVIE WASEMA 'ASANTE MAMA Na Carren Cyprian

WASANII wa Tasnia ya Filamu Tanzania (Bongo Movie) leo wamejumuika kwa pamoja na kumwambia ASANTE Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wakizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari, baadhi ya WASANII hao wamesema kuwa wanamshukuru Rais kwa kazi nzuri anayoendelea kufanya kwa Tasnia nzima ya sanaa, utamaduni na michezo.

Mmoja wa WASANII hao Steve Nyerere alisema kuwa kitendo Cha Rais kusema kuwa baadhi ya WASANII wenzao watateuliwa kuzunguka naye sehemu mbalimbali nje ya Tanzania ni wazi kuwa sekta yao imeheshimishwa.

"WASANII tutembee kifua mbele, hakuna kuwa wapole, mama ametupa heshima kubwa Sana, na sisi tuilinde heshima hiyo kwa nguvu zote," Steve.

Alisema kuwa anaamini WASANII ambao watateuliwa katika ziara hizo watalinda heshima ya WASANII wenzao na Tasnia nzima.

"Sekta ya sanaa imeajiri vijana wengi Sana ambao Kama Leo hii isingekuwa sanaa Basi wangekuwa wakabaji au mengine, hivyo kwa matarajio ya mama tutumie ziara tutakazopewa kwa umakini ili lengo ambalo mama ameliweka kwetu litimie, ikimaanisha kuongeza ujuzi na kisha kupanuka sekta yetu na kuongeza vijana wengine zadi," alisiitiza Steve.

Hivi karibuni Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema mara nyingi anapokwenda nje ya nchi huwa anafuatana na jopo la Wafanyabiashara lakini kwa sasa anataka kugeuka kidogo na atakuwa anasafiri pia na Wasanii ili kuwapa nafasi ya kujifunza zaidi kutoka nje ya Nchi na kutanua wigo wa kazi zao.

Rais Samia amesema hayo wakati akishiriki uzinduzi wa album mpya ya Msanii Harmonize.

“Tunapofungua Nchi Wageni wanakuja kwetu na sisi tunakwenda kwao na mara nyingi ninapokwenda kwao huwa nafuatana na jopo la Wafanyabiashara, sasa nataka kugeuka kidogo nataka sasa niwe nachukua Wasanii”

“Nataka nifuatane na Wasanii inategemea ratiba yangu kule nakokwenda lakini kila ninapokwenda kukiwa na matamasha ya utamaduni nitabeba Wasaniii lakini zaidi nitakuwa na safari kesho kutwa na moja ya kazi ninayokwenda kuifanya ni kutafuta nafasi za mafunzo kwa Wasanii wetu hasa Waigizaji”

Aidha katika mkutano huo WASANII hao wameibuka na msemo usemao ASANTE MAMA.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page