Na VENANCE JOHN
Bunge la nchi za Afrika Mashariki, EALA limetangaza kuwa limesimamisha vikao vyake kwa muda usiojulikana kutokana na changamoto za kifedha, zilizosababishwa na baadhi ya nchi wanachama kushindwa kulipa michango yao ya fedha. Usitishaji huo unaathiri vikao viliyokuwa vimepangwa kufanyika kuanzia Januari hadi Juni 2025.
Uamuzi huo umepitishwa kufuatia mkutano wa Kamisheni ya EALA na kamati ya viongozi ambapo washiriki waliitathmini hali ya kifedha ya bunge hilo la nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Afisa wa Mawasiliano wa EALA, Nicodemus Ajak Bior amethibitisha kwamba uhaba wa fedha umekwamisha uwezo wa bunge hilo kutekeleza kazi zake za kisheria na uangalizi.
Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC ina nchi nane wanachama zinazounda EALA, ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Randa, Burundi, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Somalia.
Comments