top of page

BUNGE LA THAILAND LAMCHAGUA BINTI WA MIAKA 37 KUWA WAZIRI MKUU

Na VENANCE JOHN


Bunge la Thailand limemchangua Paetongtarn Shinawatra kuwa waziri mkuu, mwanasiasa ambaye hana uzoefu ambaye ni mpya katika siasa ambaye pia ni waziri mkuu mdogo zaidi kuwahi kuiongoza Thailand.





Paetongtarn Shinawatra anachaguliwa baada ya aliyekuwa waziri mkuu Srettha Thavisin kuondolewa madarakani na mahakama ya katiba kwa kukiuka maadadili ya kumteua aliyewahi kufungwa jela kujumuishwa kwenye baraza la mawaziri.


Ni kijana wa miaka 37, binti wa mwanasiasa matata Thaksin Shinawatra ambaye amechaguliwa na bunge na sasa anasubiri ubatizo wa moto kupambana na siasa za nchi hiyo zenye kashikashi chungu tele.


Anakuwa waziri mkuu wa pili mwanamke nchini Thailand kuwahi kushika nafasi hiyo na wa tatu kutoka familia ya Shinawatra baada ya Shangazi yake Yingluck Shinawatra, na Baba yake Thaksin Shinawatra kuwahi kushika nyadhifa hizo.


Paetongtarn ameshinda kirahisi kwa kupata kura 319 ambazo ni karibu robo tatu ya kura zote 500 za bunge. Hakuwa ndani ya bunge wakati wa zoezi la upigaji kura na alitazama zoezi la hilo akiwa makao makuu ya chama chake cha Pheu Thai Party.


Binti huyo hajawahi kuhudumu ndani ya bunge na maamuzi ya kumweka ndani ya mchezo ni kama chama chake kimefanya mchezo wa kurusha shilingi juu na kusubiri upande utakaoangukia.


Anakwenda kupambana na changamoto rukuki mbele yake, ikiwamo uchumi unaochechemea, ushindani kutoka kwa chama hasimu cha upinzani na kushuka kwa umaarufu wa chama chake cha Pheu Thai Party.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page