top of page

BUNGE LAKANUSHA WABUNGE KUONGEZEWA MSHAHARA KUTOKA TSH MILIONI 13 HADI MILIONI 18...


Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, limetolea ufafanuzi kauli ya Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe, aliyedai kwamba mishahara ya wabunge wa Bunge hilo imeongezwa mwaka 2023 kutoka shilingi milioni kumi na tatu (13,000,000/=) hadi shilingi milioni kumi na nane (18,000,000/=).

Kupitia taarifa iliyotolewa na Bunge hilo imeeleza kuwa

hakuna Mbunge aliyeongezewa mshahara kama inavyodaiwa na

Bw. Freeman Mbowe na kwamba umma upuuze mada




hayo kwani ni uzushi na upotoshaji, na yana lengo la kuwagombanisha wananchi na wawakilishi wao ambapo taarifa hiyo imeeleza kwamba

Jana ljumaa tarehe 22 Machi, 2024 alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara Mjini Babati Mkoa wa Manyara na kisha Video yake kusambaa kwenye Mitandao ya Kijamii Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amedai kwamba mishahara ya Waheshimiwa Wabunge imeongezwa mwaka 2023 kutoka shilingi milioni kumi na tatu (sh.13,000,000/=

hadi shilingi milioni kumi na nane (sh.18,000,000/=).

Tunapenda kuujulisha umma kwamba madai hayo ni uzushi na upotoshaji kwa kuwa hakuna Mbunge aliyeongezewa mshahara kama alivyodai. Hivyo, tunapenda kuwashauri na kuwasihi wananchi kupuuza madai hayo ambayo lengo lake ni kuleta taharuki pamoja na kuwagombanisha wananchi na wawakilishi wao.

Nyongeza ya mshahara ni suala linalozingatia bajeti na hakuna utaratibu wa aina yoyote kama huo ambao umefanyika kwa ajili ya kuwaongezea Waheshimiwa Wabunge mishahara."

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page