top of page

CAMEROON: 12 WAFARIKI MAPOROMOKO YA UDONGO

Na Ester Madeghe,


Takribani watu 12 wamefariki dunia kutokana na maporomoko ya udongo magharibi mwa Cameroon siku ya Jumamosi, mamlaka ya nchi hiyo imethibitisha. Wafanyakazi wa serikali ya Cameroon, wameokoa miili 12 kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyoikumba barabara magharibi mwa Cameroon, afisa wa eneo hilo amesema, hakuna matumaini ya kupata manusura.


Televisheni ya serikali CRTV imeripoti maoni ya gavana wa mkoa wa Ouest, Augustine Awa Fonka, kuwa, "Kwa maoni yetu hakuna uwezekano tena wa kupata manusura," aliambia kituo hicho


Miili 12 imepatikana kutoka eneo lililokumbwa na maafa siku ya Jumamosi asubuhi, aliongeza kiongozi huyo Watu wengi zaidi bado hawajulikani walipo, na utafutaji wa miili bado unaendelea, aliongeza.


Maporomoko mawili ya ardhi yaligonga barabara ya Dschang cliff siku ya Jumanne, wakati wafanyakazi wa dharura walipokuwa wakitumia mashine nzito kujaribu kusafisha barabara. Magari yaliyogongwa ni pamoja na mabasi matatu yenye viti takribani 20 kila moja, magari matano ya kubeba watu sita na pikipiki kadhaa amesema Awa Fonka katika taarifa yake ya awali.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page