top of page

CCM YACHANGISHA MILIONI 5 KUSAIDIA GARI YA TUNDU LISSU ITENGENEZWE

Na VENANCE JOHN


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemchangia shilingi milioni tano Makamu Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu ili kufanya matengenezo ya gari yake.





Katibu wa NEC, itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makala ndiye aliyeendesha harambee ya kumchangia Makamu Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kiasi cha Shilingi Milioni 5.3 kwa ajili ya matengenezo ya Gari yake.


Harambee hiyo imefanyika jana, tarehe 14 Agosti 2024, kwenye Uwanja wa Furahisha, jijini Mwanza katika mkutano wa hadhara. Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema siasa si uadui hivyo ni vyema kushikana mkono pale inapobidi akisema wanasiasa wote wanalijenga taifa moja la Tanzania.

Comments

Couldn’t Load Comments
It looks like there was a technical problem. Try reconnecting or refreshing the page.
Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page