top of page

CHAMA TAWALA NCHINI UINGEREZA TUMBO JOTO Na VENANCE JOHN

Leo nchini Uiingereza wananchi wanapiga kura kwenye uchaguzi mkuu, chama tawala cha Conservative kikiwa tumbo joto kwani uchunguzi wa maoni inaonesha kuwa chama mpinzani cha Labour kina umaarufu miongoni mwa wananchi wa Uingereza. 


Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour Keir Starmer anatabiriwa kuwa atambwaga waziri mkuu wa sasa, Rishi Sunak, baada ya miaka 14 ya utawala wa chama cha Conservatives.

Uchunguzi wa maoni ya wapiga kura unaonesha kwamba Keir Starmer atapata ushindi mkubwa kutokana na wapiga kura kuchoshwa na chama tawala, ambao wameonesha kiwango cha juu cha mgawanyiko uliosababisha Uingereza kuwa na mawaziri wakuu watano ndani ya kipindi cha miaka minane.

Hata hivyo, uchunguzi huo wa maoni unaonesha kuwa wapiga kura wanataka tu mabadiliko, na sio kwamba wanakiunga mkono chama cha Labour.

Kwenye taarifa yake iliyotolewa leo, Starmer amewaambia wapiga kura kwamba huenda leo, Uingereza ikaanza ukurasa mpya, lakini amewaonya kuwa hilo litawezekana tu endapo watajitokeza kwa wingi kupiga kura.

Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page