Na Ramla Ramadhan
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dk. Hussein Ally Mwinyi amesema kwa kipindi cha miaka mingi China imekuwa mshirika muhimu katika ukuaji wa uchumi Zanzibar kupitia sekta za uwekezaji na miradi ya ujenzi wa miundombinu

Ameyasema hayo katika mkutano wa mafunzo (warsha) maalumu wa kukuza uwekezaji, Biashara na Utalii uliofanyika katika ukumbi wa mkutano Waldorf Astoria jijini Shanghai ulioandaliwa na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) kushirikiana na Ubalozi wa China, Tanzania
Mpaka sasa China ina jumla ya miradi 17 ya uwekezaji iliyosajiliwa Zanzibar yenye thamani ya takribani Dolla za Kimarekani Millioni 245 ambayo imetoa ajira za moja kwa moja kwa wananchi wa Zanzibar zipatazo 8,000
Pia China ni mshirika wa pili katika ukubwa kwenye Sekta ya Biashara Zanzibar ambapo thamani ya biashara katika Nchi hizo mbili imepanda kwa mwaka 2023 hadi kufikia Dola Millioni 66.5 na kukuza sekta ya Kilimo na viwanda
Mkutano huo ni hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano baina ya Nchi hizo mbili katika maendeleo ya Nchi hususani uchumi na uwekezaji, kubadilishana fursa za biashara pamoja na teknolojia.
Commentaires